Je, hisa za kijani ni upepo mpya wa soko la fedha Tanzania?
Katika ulimwengu unaobadilika kwa kasi, ambapo mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira vimekuwa changamoto kubwa, dhana ya fedha endelevu imepata umaarufu mkubwa. Fedha endelevu inahusu uwekezaji na mifumo ya kifedha inayozingatia masuala ya kimazingira, kijamii na utawala bora (ESG – Environmental, Social, and Governance). Tanzania, kama nchi nyingine zinazoendelea, inakabiliwa na uhitaji mkubwa wa…