
Nyumba 76 za watumishi wa afya, zitakavyoboresha utoaji huduma
Unguja. Familia 76 zimepata makazi karibu na Hospitali ya Rufaa ya Abdalla Mzee, Kusini Pemba hatua inayotajwa kuongeza ufanisi wa kutoa huduma katika hospitali hiyo baada ya kuwaepusha wataalamu kutembea masafa marefu kwenda kutoa huduma. Nyumba hizo 76 zenye gharama ya Sh16.481 bilioni zimejengwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na kuikabidhi Serikali…