
Kada CCM aliyemwagiwa tindikali aandika barua THBUB, ajibiwa
Moshi. Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Idrisa Moses maarufu Makishe, ameiandikia barua Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), akiiomba kuanza uchunguzi huru kuhusu tukio la kumwagiwa tindikali. Septemba 20, 2024 saa 2:00 usiku, watu wasiojulikana walimmwagia Makishe ambaye ni mkazi wa mjini Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro kimiminika kinachodhaniwa ni tindikali na…