
Wanne wana kesi ya kujibu mauaji ya Milembe
Geita. Washtakiwa wanne kati ya watano wanaodaiwa kumuua Milembe Suleman (43), wamekutwa na kesi ya kujibu na wataanza kujitetea kesho Juni 28, 2024. Akitoa uamuzi baada ya upande wa Jamhuri kuomba kufunga ushahidi wake kutoka kwa mashahidi 29 na vielezo 19, Jaji wa Mahakama hiyo, Kelvin Mhina amesema kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa, washtakiwa wanne…