
Ruto asikia kilio cha Gen Z, aurudisha Muswada bungeni
Nairobi. Baada ya wiki mbili za maandamano na ghasia nchini Kenya, hatimaye Rais wa nchi hiyo, William Ruto ametangaza kuondoa Muswada wa Fedha wa mwaka 2024, akisema licha ya kuwa na nia njema, wananchi wameonyesha kuukataa. Maandamano hayo yalishika kasi jana Jumanne Juni 25, 2024 baada ya waandamanaji kuvamia majengo ya bunge, dakika chache baada…