
MTANZANIA WA DIASPORA ABDALLAH NYALIGWA ACHUKUA FOMU UBUNGE ITWANGI
Mtanzania anayeishi Uingereza, Abdallah Nyaligwa, leo Juni 30,2025 amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania Ubunge wa Jimbo Jipya la Itwangi, ambalo limegawanywa kutoka Jimbo la Solwa. Nyaligwa mzaliwa wa Itwangi kutoka familia ya Chief Kaswende Shikira anakuja kuwania nafasi hii akiwa na kumbukumbu ya heshima na urithi wa familia…