
Wastaafu waliopunjwa mafao watangaziwa neema
Dodoma. Serikali imetangaza habari njema kwa wastaafu waliostaafu kuanzia Julai mwaka 2022, ambao ni 17,068 kuwa watalipwa mapunjo yao ya mafao ya mkupuo kulingana na kikotoo kilichotangazwa Juni 13, 2024. Kiasi cha mafao ya mkupuo kiliongezwa kutoka asilimia 33 hadi 40 kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na 33 watapata…