


RAIS SAMIA AKUTUNA NA KUZUNGUMZA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA DJIBOUT IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Mjumbe Maalum wa Rais wa Djibouti Mhe. Ismail Omar Guelleh ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Mahmoud Ali Youssouf mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Januari, 2025.

Bashe: Kilimo ni Sayansi na Igunga imekuwa kinara cha uzalishaji P
*Serikali haiwezi kuleta dawa na mbegu bandia Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, ameongea na Wakulima wa zao la Pamba katika Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora na kusema kuwa kilimo ni sayansi na kinahitaji tija na ubora na hiyo imekuwa dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mbegu bure,…

TIA Yasaini Mkataba na Kampuni ya Salem Construction Kwaajili ya ujenzi wa jengo kampasi ya Singida – MWANAHARAKATI MZALENDO
TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA), imesaini mkataba na kampuni ya Salem Construction kwaajili ujenzi wa jengo la kampasi yake mkoani Singida ambapo mkataba huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 13.5. Mkataba huo utachukua miezi 24 hadi kukamilika kwa ujenzi jengo hilo mkoani Singida. Akizungumza leo Oktoba 15,2024 katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ofisi za taasisi…

Mwenezi CPA Makalla apokelewa mkoani Arusha tayari kwa kuanza ziara yake
Katibu wa NEC, itikadi, uenezi na mafunzo Ndugu Amos Makalla amewasili tayari kuanza ziara yake ya siku 6 katika mkoa wa Arusha na Manyara. makalla amepokelewa na mwenyekiti wa ccm mkoa wa arusha ndugu loy thomas sabaya pamoja na viongozi wa chama mkoa wa arusha. CPA Amos Makalla akiwa mkoani Arusha atazungumza na wananchi kwenye…

Mahakama yawashushia rungu IGP, DPP watuhumiwa kushikiliwa kwa siku 15
Bukoba. Mahakama Kuu ya Tanzania, imewaamuru Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kuwaachia au kuwafikisha kortini, watuhumiwa wanne wanaowashikilia mahabusu ya polisi kwa siku 15. Amri hiyo imetolewa leo Jumatano Juni 26, 2024 na Jaji Gabriel Malata wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba wakati akitoa uamuzi wa maombi ya jinai…

Mwenyekiti wa kitongoji wa Chadema atimkia CCM
Rombo. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kitowo kilichopo katika Kijiji cha Mengwe Juu, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Agustina Lyakurwa amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kukaa kwenye nafasi hiyo kwa takribani siku 25 baada ya kuchaguliwa Novemba 27, 2024. Hicho ndicho kitongoji pekee kilichochukuliwa na…

Wanawake waongoza mashauri ya ndoa, familia
Dar es Salaam. Wanawake wametajwa kuwa mstari wa mbele kuripoti mashauri ya ndoa na kifamilia kuliko wanaume, sababu zikiwa ni ongezeko la talaka, kutafuta mirathi na matunzo ya watoto. Hayo yamo kwenye ripoti ya msaada wa kisheria ya mwaka 2023 iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) leo Jumanne Agosti 20, 2024…

Wanaume wanavyokufa na tai shingoni
Wanaume wamekuwa wakielemewa na matatizo ya msongo wa mawazo kutokana na changamoto za kikazi na kifamilia. Hata hivyo, imebainika kuwa wengi wao huchelea kufichua matatizo yao kwa wenzao kazini au watu wa familia zao. Hii ndiyo maana miongozo ya kiserikali inawahitaji waajiri kutekeleza mipango ya kuwasaidia wafanyakazi kukabiliana na hali zinazoweza kuwasababishia msongo wa kiakili….

MSOMERA WAMSHKURU RAIS SAMIA – Mzalendo
Wakazi wa Kijiji cha Msomera, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wamemshkuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo mbalimbali na uboreshwaji wa huduma katika kijiji hicho. Kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais, Dk. Samia imefanya maendeleo makubwa katika kijiji…