
Viongozi wengine Chadema Dar watimka, watangaza kugombea ubunge
Dar es Salaam. Bado hamahama ya wanachama ndani ya Chadema imeendelea kushika kasi baada ya makada wengine watano kujiondoa huku wakisema wanakwenda kutafuta majukwaa mengine ili wapate nafasi ya kuwawakilisha wananchi wao kwenye vyombo vya kufanya uamuzi. Wanachama waliojiengua leo Jumatano, Mei 14, 2025 ni Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa kichama Kinondoni, Henry Kileo na…