
CCM, Ikulu Zanzibar waikana kauli ya Dk Dimwa
Dar es Salaam. Hapana. Ndivyo unavyoweza kutafsiri karibu kila mchango wa mdau wa siasa aliyezungumza na Mwananchi kuhusu kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk Mohamed Dimwa, aliyetaka Rais Hussein Mwinyi aongezewe muda wa kukaa madarakani kutoka miaka mitano hadi saba. Msingi wa kauli hiyo ya Dimwa ni kile alichoeleza…