
NJE YA UWANJA: Yanga, Simba zinabebwa na haya
Soka la Tanzania kwa upande wa klabu limetawaliwa zaidi na timu za Simba na Yanga. Hilo lipo wazi kwani hata ukiangalia listi ya mabingwa wa Ligi Kuu utapata jibu lisilokuwa na shaka ndani yake. Tangu mwaka 1965 ilipoanza ligi hiyo, Yanga na Simba ndiyo timu zinazoongoza kwa kubeba ubingwa mara nyingi Zaidi. Yanga ikiwa kinara…