ADC yaahidi mapinduzi ya kilimo, mikopo, miundombinu na kodi

Simiyu. Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaoa kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Wilson Mulumbe, ameahidi kujenga kiwanda cha vifaa tiba mkoani Simiyu kwa lengo la kuongeza thamani ya zao la pamba, endapo kitashinda katika uchaguzi mkuu ujao. Akizungumza leo, Jumatano, Septemba 10, 2025, mjini Bariadi, Mulumbe amesema lengo la kiwanda…

Read More

Mtihani mwingine Ibenge, Folz Bara

LEO Jumatano, Kocha wa Azam, Florent Ibenge na wa Yanga, Romain Folz, wanaanza kibarua cha kuziongoza timu hizo katika Ligi Kuu Bara. Makocha hao wanaingia uwanjani wakiwa wametoka kupata ushindi muhimu ugenini kwenye mashindano yanayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) upande wa ngazi ya klabu. Azam itaikaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa…

Read More

Sababu na athari ndoa za siri

Ndoa ni muunganiko rasmi wa watu wawili wanaopendana, kwa lengo la kuishi pamoja kwa upendo, heshima, na mshikamano.  Kikawaida, ndoa hufanyika kwa uwazi na kushuhudiwa na familia, jamii na mamlaka husika kama taasisi za dini au serikali.  Hata hivyo, uzoefu hivi sasa unaonyesha, kuna ongezeko la ndoa zinazofungwa kwa siri, yaani, ndoa ambazo hufanyika kwa…

Read More

Mawakili waketi wakiwasubiri majaji kesi ya Mpina

Dodoma. Mawakili wa Chama cha ACT -Wazalendo na wale wa Serikali wameshaingia na kuketi kwenye viti vyao mahakamani tayari kwa ajili ya kesi ya Luhaga Mpina aliyeenguliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Leo Jumatatu Septemba 8, 2025 katika Mahakama Kuu Masijala Kuu-…

Read More

Gamondi  aanza na sare Kagame 

KOCHA Miguel Gamondi ameanza na sare akiwa na Singida Black Stars kwenye mashindano ya Kombe la Cecafa Kagame dhidi ya Ethiopian Coffee kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo. Katika mechi hiyo ya kwanza ya kimashindano kwa kocha huyo aliyewahi kuifundisha Yanga, tangu apewa mikoba ya kuongoza kikosi hicho, Singida BS ilionekana kutokuwa na makali katika…

Read More

Polisi waendelea kumsaka mganga anayedaiwa chanzo cha kifo cha mwanafunzi

Arusha. Zikiwa zimepita siku 17 tangu kufariki dunia kwa mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Qash iliyopo wilayani Babati, mkoani Manyara, Yohana Konki (17), Jeshi la Polisi mkoani Manyara limesema linaendelea kumsaka mganga wa kienyeji anayedaiwa kutoa ramli chonganishi iliyosababisha mauaji hayo. Yohana, alifariki dunia baada ya kupigwa na wanafunzi wenzake kwa…

Read More

Biashara ya maziwa inavyowainua kiuchumi wanawake wa Mwika

Moshi. Wakati changamoto ya ajira ikiendelea kuwa kikwazo nchini, baadhi ya wanawake wa Kata ya Mwika Kaskazini, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wameeleza namna shughuli ya uuzaji wa maziwa ya ng’ombe inavyowainua kiuchumi na kuboresha maisha ya familia zao. Wanawake hao ambao wamejikita katika ufugaji wa ng’ombe wa maziwa na kuuza maziwa  katika kiwanda cha…

Read More