
WANANCHI 851 KULIPWA FIDIA YA ZAIDI YA BILIONI 5 KUPISHA UJENZI WA BARABARA YA LIKUYUFUSI-MKENDA MKOANI RUVUMA
NA BELINDA JOSEPH, SONGEA. Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Ruvuma umewahakikishia wananchi 851 waliopisha mradi wa ujenzi wa barabara ya Likuyufusi-Mkenda kuwa watalipwa fidia mapema bila kuathiri shughuli zao za kiuchumi na kijamii. Fidia hiyo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 5 inatarajiwa kulipwa mara baada ya TANROADS kupokea fedha kutoka Wizara…