MBUNGE KISHIMBA AITAKA SERIKALI KUREKEBISHA BARABARA MBOVU ZIKIZOPO KAHAMA MJINI

Na Janeth Raphael- MichuziTv – Bungeni Dodoma Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kishimba ameiomba serikali kuimarisha miundo mbinu ya barabara katika jimbo lake Kahama Mjini Mkoani Shinyanga ambayo imeharibika kwa kiasi kikubwa ili kuchochea wafanyabiashara kuendelea kulipa kodi na kufanya biashara katika mazingira rafiki. Mbunge huyo ametoa kauli hiyo Bungeni Jijini Dodoma…

Read More

MSONDE AWATAKA WARATIBU WA TASAF KUSIMAMIA MRADI KWA WELEDI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde amewataka wasimamizi wa Mradi wa Kupunguza Umaskini TASAF awamu ya nne kusimamia Mradi huo kwa weledi na kuhakikisha utekelezaji wa mradi huo unakuwa kama ilivyokusudiwa. Dkt. Msonde ametoa maelekezo hayo mkoani Mwanza wakati akifungua kikao kazi cha mradi wa kupunguza umasikini awamu ya…

Read More

Askofu Wolfang Rais mpya TEC, Padri Kitima aula tena

BARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetambulisha safu mpya za viongozi watakaoongoza baraza hilo kwa miaka mitatu hadi 2027 huku aliyekuwa Katibu Mkuu wa baraza hilo, Padri Dk. Charles Kitima akirejeshwa tena kuendelea kutumikia nafasi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Baraza hilo limemtambulisha Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa OFM Cap ambaye ni Askofu wa Jimbo…

Read More

Boti za kisasa zaongeza uvuvi wa samaki Ziwa Victoria

Mwanza. Uzalishaji wa samaki kwa baadhi ya wavuvi wa Ziwa Victoria umeongezeka kutoka kilo 20 kufikia kilo 300 kwa wiki, baada ya kuanza kutumia boti za kisasa walizokopeshwa na Serikali. Hiyo imefanya uzalishaji huo kuwaingizia Sh3 milioni kutoka Sh200,000 baada ya kuuza kilo moja ya samaki  kwa Sh10,000. Januari 30, 2024 Rais Samia Suluhu Hassan…

Read More

Jokate awananga vijana wabebao mabegi ya wagombea

Iringa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Jokate Mwegelo amewataka vijana kutotumika vibaya kubeba mabegi ya watu wanaotaka kugombea katika nafasi mbalimbali,  kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu hapo mwakani. Amesema badala ya kutumika vibaya, vijana hao wanapaswa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali na kwamba wapo tayari…

Read More

Ustaadh matatani madai ya kumfanyia ukatili mwanawe

Musoma. Ustaadh wa msikiti wa Aljazeera uliopo katika Mtaa wa Nyabisare, manispaa ya Musoma mkoani Mara ameingia matatani kwa tuhuma za kumfanyia ukatili na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili mtoto wake wa kumzaa. Ustaadh huyo, Issa Mgema (30) anadaiwa kumfanyia ukatili kwa kumpiga na kumchapa na waya wa umeme sehemu mbalimbali za mwili mtoto huyo…

Read More

Uwanja wa ndege watajwa kuifungua Mbarali kiuchumi

Mbeya. Kuwapo kwa uwanja wa ndege katika kijiji cha Mulungu kilichopo Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya,  kumetajwa kuinua uchumi na kufungua fursa za ajira kwa vijana hasa kwenye sekta ya utalii. Uwanja huo wenye urefu wa kilomita 1.2 ambao umezinduliwa Juni 20, umejengwa na Serikali kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Hifadhi ya Taifa…

Read More

NYUMA YA PAZIA: Komasava na saluti zote kwa Ng’olo Kante

ALIONDOKA uwanjani na kitambaa katika bega kama nahodha, tabasamu usoni. Sura chini. Mfupi kama alivyo, shujaa kama alivyo, N’Golo Kante alinikumbusha mbali katika pambano la majuzi kati ya Ufaransa dhidi ya Austria kule Ujeumani. Kwamba N’Golo ni yule yule tu. Baada ya pambano aliingia katika vyumba vya kubadilishia nguo na wachezaji wenzake wakaanza kumshangilia. Mchezaji…

Read More