
Mbinu ya kuharakisha matumizi nishati safi yatajwa
Dar es Salaam. Katika kuharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini Tanzania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji ya Maendeleo (UNCDF) limependekeza ushirikishwaji wa viongozi wa dini na wale wa kimila katika kutoa elimu kwa wananchi. Pendekezo hilo limetolewa leo Juni 21, 2024 na Ofisa Mwekezaji Mwandamizi wa UNCDF, Emmanuel Muro, katika kongamano…