Waziri Masauni afunguka mapya watuhumiwa ‘waliotumwa na afande’
Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Hamad Masauni amesema mchakato wa kuwakamata watuhumiwa wanaodaiwa kumbaka na kumlawiti msichana, anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Dovya, Mkoa wa Dar es Salaam, unaendelea. Kauli ya Masauni ni mwitikio wa tukio la video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikionyesha vijana watano wakidaiwa wakimbaka na kumwingilia…