
Mahakimu watatu wanavyopambana kudai haki kortini
Dodoma. Mahakama Kuu, imewapa kibali, mahakimu watatu wa zamani wa mhimili huo, ili wafungue maombi ya kuomba kurejewa kwa uamuzi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wa kuwafuta kazi na hatimaye kubatilisha uamuzi huo. Uamuzi wa kuwaruhusu mahakimu hao wa zamani kufungua maombi hayo, ulitolewa Juni 18, 2024 na Jaji Fredrick Manyanda wa Mahakama Kuu…