
Vilio, simanzi vyatawala nyumbani kwa RAS Kilimanjaro
Moshi. Vilio na simanzi vimetawala nyumbani kwa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Tixon Nzunda (56) aliyefariki kwa ajali ya gari yeye na dereva wake wakati mwili huo ulipowasili nyumbani kwake Shanty Town, Manispaa ya Moshi, mkoani humo, saa 4:50 asubuhi, ukitokea Hospitali ya KCMC ulikokuwa umehifadhiwa. Tixon yeye na dereva wake, Alphonce Edson…