
NMB, IFC na Mastercard Waingia Makubaliano Kuboresha Upatikanaji wa Huduma za Kifedha kwa Wanawake Nchini.
Washington, DC, Marekani. Benki ya NMB imesaini makubaliano na Shirika la Kimataifa la Fedha (IFC) na Mastercard kuzindua Mradi wa Ushauri wa “Banking on Women Advisory Project,” ambao unalenga kuboresha masuluhisho ya kifedha kwa wanawake nchini Tanzania. Makubaliano hayo yamesainiwa siku ya Alhamisi, tarehe 24 Oktoba 2024, katika Mkutano wa Mwaka wa Shirika la IFC…