
Kamatakamata ya ‘makahaba’ Dar yadaiwa kukiuka haki ya faragha
Dar es Salaam. Sakata la ukamataji wanawake wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya ukahaba, limeibua mjadala kutoka kwa wanaharakati. Ukamataji huo pia unahusisha wanaume wanaokuwa na wanawake hao bila kujali kama wanahusika ama la. Hata hivyo, uchunguzi wa Mwananchi umebaini licha ya ukamataji kufanyika, bado hurejea katika maeneo hayo na kuendelea na shughuli zao kama kawaida….