
Polisi ilivyobadili mbinu kudhibiti waumini kanisa la Askofu Gwajima
Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imebadili mbinu ya kuwadhibiti waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima. Tofauti na awali, tangu kanisa hilo lilipotangazwa kufutwa na polisi kulizungushia utepe kuashiria kutoruhusu waumini kuendelea na ibada, leo Jumapili Juni 22, 2025 utaratibu wa ulinzi kanisani hapo umebadilika….