


TETESI ZA USAJILI BONGO: Ibenge kuitibulia Simba SC kwa Pokou
KLABU ya Al Hilal ya Sudan imeingilia kati dili la kiungo Serge Pokou wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast ambaye pia amekuwa akiwindwa na Simba. Vigogo hao wamedhamiria kufanya usajili wa maana katika dirisha hili la usajili kwa ajili ya kujiimarisha na michuano ya kimataifa msimu ujao. Simba ipo kwenye mazungumzo na beki wa kati…

BRELA “unaweza kupata Leseni popote kikubwa mtandao”
Katika kuhakikisha wanaendelea kurahisisha utoaji huduma Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umesema kupitia mfumo wa kimtandao wa ORS unaoweza kupata huduma zao zikiwemo za kufanya sajili za kibiashara kama leseni ya kiwanda au kusajili ukiwa kokote kule hata kama utakuwa kitandani. Hayo yamesemwa na Endrew Mkapa ambaye ni Mkurugenzi wa Leseni kutoka…

Rais Putin azuru Vietnam, nini kinatarajiwa huko? – DW – 19.06.2024
Rais Putin anazuru mji mkuu wa Vietnam kwa mwaliko wa Katibu Mkuu Chama cha Kikomunisti nchini Vietnam Nguyen Phu Trong. Nchi hiyo inatarajia nini kutoka kwa Putin ambaye pamoja na mengineyo anakabiliwa na vizuizi na waranti wa kukamatwa wa mahakama ya ICC? Kesho Alhamisi, Rais Vladimir Putin atakaribishwa rasmi katika hafla itakayofanyika kwenye Makazi ya…

Wabunge wapinga ongezeko la Sh382 bei ya gesi
Dodoma. Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wameitaka Serikali kuondoa ongezeko la Sh382 kwenye bei ya gesi inayotumika kwenye magari badala yake iongeze vituo vya utoaji wa gesi na kuweka ruzuku kwenye vifaa vya matumizi ya gesi. Wamesema hayo wakichangia makadirio ya bajaeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ambapo…

Siku 14 nzito za Simba
KUNA kipindi kizito cha takribani siku 14 walichonacho Simba SC chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ambaye pia ni Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’. Simba SC ambayo hivi karibuni ilipata mtikisiko kidogo wa baadhi ya viongozi wake wa Bodi ya Wakurugenzi upande wa Mwekezaji kujiuzulu wote akiwemo Salim Abdallah ‘Tyr…

WAZIRI SIMBACHAWENE AIPONGEZA EWURA KATIKA MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene,akisoma moja ya kipeperushi chenye ujumbe kuhusu EWURA wakati alipotembelea banda la EWURA wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma. WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa…

Hifadhi ya Mikumi Yatoa Madawati 213 shule za msingi 7.
Katika kuendelea Kuunga mkono juhudu za serikali Kwenye sekta ya elimu Hifadhi ya Taifa Mikumi imetoa msaada wa Madawati Kwenye Shule za msingi saba zinazozunguka Hifadhi hiyo kwenye kata za Mhenda,Ruhembe na Mikumi. Akizungunza katika hafla ya kukabidhi Madawati kaimu Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa Mikumi. Afisa mwandamizi wa uhifadhi Buka Alfred amesema wametoa madawati…

Ramaphosa aapishwa kuanza muhula wa pili Afrika Kusini – DW – 19.06.2024
Halfa ya taifa ya kumwapisha Ramaphosa imefanyika kwenye mji mkuu wa serikali ya nchi hiyo Pretoria na kuhudhuriwa na viongozi wa mataifa kadhaa ya Afrika. Kiapo cha urais kiliongozwa na Jaji Mkuu wa Afrika Kusini Raymond Zondo mbele ya majengo ya Ikulu ya nchi hiyo. Mfalme Mswati III wa Ufalme wa Eswatini, Rais Samia Suluhu…

Mahakama yabatilisha kifungo cha miaka 20 jela kwa aliyedaiwa kusafirisha mirungi
Arusha. Mahakama ya Rufani nchini imebatilisha mwenendo wa kesi na kufuta hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela aliyohukumiwa Mussa Bakari, aliyetiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha kilo 109.17 za mirungi. Aidha, mahakama hiyo imeamuru kesi hiyo isikilizwe upya na mahakama yenye uwezo baada ya kupata kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) na…