
Lissu, wafuasi waonywa kutaja ‘No reforms, no election’ mahakamani
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amezua jambo baada ya kutamka kaulimbiu ya chama hicho kupinga uchaguzi ya ‘No reforms, no election’ akiwa kizimbani mbele ya hakimu na kusababisha Mahakama hiyo kumpa onyo. Lissu ametamka kaulimbiu hiyo baada kupanda kizimbani katika kesi ya uhaini inayomkabili, leo Jumatatu, Juni…