
Watumishi watatu waadhibiwa Longido, mmoja afukuzwa kazi
Arusha. Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha, limetoa adhabu kwa watumishi wake watatu wa halmashauri hiyo, akiwemo mmoja kufukuzwa kazi. Mtumishi mwingine ameshushwa cheo na mwingine ameadhibiwa kupunguziwa mshahara wake kwa asilimia 15 kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kutokana na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh300 milioni….