
Kigoda cha taaluma cha Sheikh Karume chazinduliwa
Unguja. Wakati kikizinduliwa Kigoda cha taaluma cha Sheikh Abeid Amani Karume katika ukombozi wa maendeleo ya Afrika, Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi na marais wastaafu wameeleza umuhimu wa vigoda, wakisisitiza kujikita katika kufanya tafiti. Kigoda hicho kimezinduliwa leo Juni 15, 2024 na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi, katika Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar…