Mtazamo kufungwa mtandao wa X wazua mjadala mzito

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) na baadhi ya viongozi wa dini kutoa matamko ya kuiomba Serikali iufungie mtandao wa X (zamani Twitter), baadhi ya wadau wamepinga vikali ombi hilo wakisema ni ukiukwaji wa haki ya uhuru wa kujieleza na kutoa maoni. Hata hivyo,…

Read More

WAKURUGENZI, MAAFISA ELIMU NA MAAFISA UTUMISHI SHIRIKIANENI KUTATUA KERO ZA WALIMU NCHINI

Naibu katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu) Dkt Charles Msonde amewaelekeza wakurugenzi wa Halmashauri kote nchini kushirikiana na maafisa Elilmu na maafisa Utumishi wa Halmashauri kutatua kero mbali mbali zinazowakabili walimu kote nchini. Dkt. Msonde ametoa maelekezo hayo katika kikao cha Pamoja kati ya walimu wa shule za msingi na sekondari, Wakuu wa Shule…

Read More

Marekani yasaka fursa uwekezaji sekta ya nishati Tanzania

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amekutana na Naibu Waziri wa Nishati wa Marekani, David Turk kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji katika sekta ya nishati nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea). Mkutano huo umefanyika leo tarehe 12 Juni 2024 jijini Dar es Salaam na kubainisha maeneo kadhaa ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na…

Read More

Safari treni ya SGR kuanza Dar-Moro Juni 14

Dar es Salaam. Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kuanza kwa safari za treni ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kuanzia Ijumaa ya Juni 14, 2024. Kuanza kwa safari hizo kunafanyika karibu wiki mbili kabla ya siku ambayo Rais Samia Suluhu Hassan atazindua rasmi safari ya treni hiyo, Juni 25, mwaka huu….

Read More

SPOTI DOKTA: Stars walikuwa timamu

USIKU wa Jumanne ulikuwa mzuri kwa timu ya taifa, Taifa Stars mara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Zambia ndani ya dimba la Levy Mwanawasa katika jiji la Ndola. Kwa ushindi huo wa bao la mapema dakika ya 5 lililofungwa na Waziri Junior Shentembo unaiweka Taifa Stars…

Read More

Dk Mwinyi: Mazingira mazuri yamewavutia wawekezaji

Unguja. Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi amesema mazingira mazuri na miundombinu bora ndio inamfanya mwekezaji kuwekeza fedha zake, hivyo Serikali itafanya kila linalowezekana kuendelea kuboresha mazingira kukuza uchumi. Dk Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Jumatano Juni 12, 2024 wakati akizindua Hoteli ya The Mora inayomilikiwa na Kampuni ya Tui Group Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja. Katika kuhakikisha…

Read More

KITUO CHA POLISI MKIWA KUKAMILIKA

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameihoji serikali ni lini itaunga mkono jitihada za wananchi,wadau na Mbunge kupitia mfuko wa Jimbo katika ujenzi wa Kituo kidogo cha Polisi kilichopo Kata ya Mkiwa ili kituo hicho kikamilike na kisaidie kuimarisha usalama wa wananchi. Mtaturu ameuliza swali hilo Juni 12,2024,Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na…

Read More