


BODI YA UTALII TANZANIA YAWAKARIBISHA MA-CEO ARUSHA KUSHIRIKI KIKAO KAZI,AWAOMBA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII VILIVYOPO
Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru, amewakaribisha rasmi wageni na washiriki wote wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma (CEOs Forum 2025) kitakachofanyika kuanzia Agosti 23 hadi 26 , 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC, jijini Arusha. Amesema…

Rais Samia Aongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM – Global Publishers
Dodoma, Agosti 23, 2025 – Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika mkoani Dodoma. Kikao hicho kilijumuisha viongozi wakuu wa chama na kililenga kushughulikia masuala muhimu ya kitaifa na ya ndani…

SERIKALI YAWEZESHA HUDUMA ZA POSTA KIDIJITALI KUPITIA VIFAA VYA TEHAMA KUTOKA UCSAF
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa, amesema Serikali ya Awamu ya Sita imejipanga kuhakikisha huduma za msingi ikiwemo Posta, Mawasiliano, intaneti na huduma za kifedha za kidijitali zinawafikia wananchi wote bila kujali jiografia. Waziri Silaa aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, Agosti 22, 2025, katika hafla ya makabidhiano ya vifaa vya…

Wanandoa wauawa kikatili, miili yachomwa moto
Mbeya. Wanandoa wanaodaiwa kuwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wameuawa katika Kijiji cha Chafuma, wilayani Momba. Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Jeshi la Polisi Agosti 23, 2025 tukio la mauaji lilitokea Kata ya Kapele iliyo Tarafa ya Ndalambo, juzi Agosti 22, saa nane mchana. Taarifa hiyo iliyotolewa na Kamanda…

Wasiojulikana wajeruhi, watoweka na Sh20 milioni
Same. Watu wasiojulikana wamemvamia na kumjeruhi kwa mapanga Yusto Mapande, mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro. Mapande alijeruhiwa alipokuwa akiingia nyumbani kwake akitokea kwenye biashara zake, pia ameporwa zaidi ya Sh20 milioni zilizokuwa kwenye gari lake. Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amethibitisha tukio hilo akisema limetokea jana Agosti 22,…

Mgogoro wa ardhi kati ya wananchi, mgodi wa GGML wamalizika
Geita. Mgogoro uliodumu kwa miaka 26 kati ya wananchi wa mitaa ya Nyakabale na Nyamalembo na Mgodi wa Uchimbaji Madini wa Geita (GGML) hatimaye umefikia tamati, baada ya kampuni hiyo kukubali kuwalipa fidia wananchi ili waondoke na kupisha shughuli za uchimbajii. Mgogoro huo ulitokana na wananchi kuishi ndani ya vigingi vya leseni ya uchimbaji, jambo…

Hekaya za malevi: Akili mnemba kizibo cha akili – 2
Dar es Salaam. Siwezi kubishana na umati unaodai kuwa akili mnemba ni maendeleo. Hoja yangu ni lugha inayotumika tukisema “Maendeleo ni kutoka mahala na kwenda mahala pengine”, haimaanishi kwenda kinyumenyume ni maendeleo. Hivyo nakusudia kusema kuwa matumizi ya akili mnemba bado hayajaeleweka sawasawa miongoni mwa watumiaji wake. Wanaiweka mbele wakidhani kuwa ina silika za ufundishaji….

Rais mstaafu Sri Lanka atupwa sero kwa matumizi mabaya ya fedha
Idara ya Upelelezi wa Jinai (CID) nchini Sri Lanka imemkata aliyekuwa Rais wa zamani wa Taifa hilo, Ranil Wickremesinghe kwa madai ya matumizi mabaya ya fedha za Serikali. Wickremesinghe (76) amekamatwa baada ya kufika katika ofisi ya CID katika mji mkuu Colombo kutoa maelezo ya taarifa ya uchunguzi wa ziara yake ya London pamoja kuhudhuria…

VIDEO: Kutoka kukata tamaa hadi matumaini tiba ya moyo
Dar es Salaam. Miaka 15 iliyopita, kupata ugonjwa wa moyo nchini Tanzania kulikuwa ni kama hukumu iliyoambatana na gharama kubwa kifedha, safari ndefu kwenda nje ya nchi au kukata tamaa ya matibabu na kupona. Kabla ya mwaka 2008, upasuaji mkubwa wa moyo haukufanyika nchini, hivyo iliwalazimu wagonjwa kusafiri hadi India na mataifa mengine kupata tiba;…