Kocha Simba hakamatiki Rwanda | Mwanaspoti
ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, ameendelea kuonyesha umahiri wake wa kiufundi Ukanda wa Afrika Mashariki akiwa na Rayon Sports ya Rwanda. Kocha huyo amekuwa na mwanzo mzuri wa msimu, akiiongoza timu hiyo kuvuna pointi 23 katika mechi tisa za Ligi Kuu Rwanda ikishinda saba na sare mbili. Chini ya uongozi wake, Rayon…