KURA 7,092 ZA MPA UBUNGE ‘PELE’ JIMBO LA KWAHANI

Mbunge mteule wa Jimbo la Kwahani Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharib, Zanzibar, Bw.Khamis Yussuf Mussa akinyanyua juu hati yake ya ushindi baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi. Mbunge mteule wa Jimbo la Kwahani Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharib, Zanzibar, Bw.Khamis Yussuf Mussa akionesha hati yake ya ushindi baada ya kukabidhiwa…

Read More

Kundemba yaizima JKU, Malindi ikizinduka ZPL

VINARA wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL), JKU jana ilijikita ikisimamishwa na Kundemba kwa kulimwa mabao 2-0 katika mechi za lala salama za Ligi hiyo, huku Malindi ikizinduka kwa Uhamiaji. JKU inayoongoza msimamo wa Ligi ikihitaji pointi mbili tu itangaze ubingwa mapema, ilikumbana na kipigo hicho kwenye Uwanja wa Mao A, mjini Unguja. Kipigo hicho kimeiacha…

Read More

Wawakilishi watilia shaka bajeti uchumi wa buluu

Unguja. Wakati bajeti ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ikipitishwa, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamesema bado hawajaona mkakati madhubuti wa kutekeleza sera ya uchumi wa buluu. Bajeti hiyo ya Sh66 bilioni imepitishwa na Baraza Juni 8, 2024 ikiwa na vipaumbele 12. Mwakilishi wa Pandani, Profesa Omar Fakih Hamad amesema wizara hiyo ndiyo…

Read More

Mama wa mtoto mwenye ualbino aliyeibiwa aliangukia Jeshi la Polisi

Muleba. Judith Richard (20), Mama mzazi wa mtoto mwenye ualbino,  Asimwe Novath (2) aliyeibiwa na watu wasiojulikana akiwa sebuleni kwao Kitongoji cha Mbale Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, ameliomba Jeshi la Polisi kuwabana watuhumiwa linaowashikilia ili waseme mtoto wake alipo. Mama huyo amedai kuwa miongoni mwa wanaoshikiliwa yupo aliyemchukua mtoto wake siku 10 zilizopita ndani…

Read More