
KONA YA WASTAAFU: Nyongeza ya Pensheni ya wastaafu inapooteshwa mbawa!
Oktoba 2024, iliyopita, siri-kali ilijikanyaga katika kile ilichookita ni kumsaidia mstaafu wake wa Kima cha Chizi kuweza kukabiliana na hali ngumu ya maisha iliyokuwa ikimkabili. Ilimtangazia mstaafu huyo nyongeza ya pensheni ya Sh50,000 ambayo ukiongeza na ile laki moja kwa mwezi aliyokuwa akipata kwa miaka 21 nyuma, angekuwa sasa akipata Sh150,000. Siri-kali haikulazimishwa na yoyote….