
Chadema yabadili gia angani kisa Golugwa kuzuiwa, yamtumia mke wa Lissu
Meatu. Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimefanikiwa kuwasilisha taarifa ya hali ya kisiasa nchini katika mkutano wa Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Duniani (IDU) unaofanyika mjini Brussels, Ubelgiji, licha ya Jeshi la Polisi kumkamata na kumzuia Naibu Katibu Mkuu wao, Amani Golugwa kuhudhuria mkutano huo. Akihutubia mkutano wa hadhara mjini Mwanhuzi wilayani Meatu leo…