
Mafyatu kumkaribisha Rahis kuzindua kijiwe
Baada ya kuona kuwa inawezekana kumfyatua, sorry, kumchengua rahis hadi anazindua mangomangoma ya Hamnazoo, mafyatu tunakula mkakati kumkaribisha kuzindua kijiwe chetu cha ndumuu. Naona yule anatikisa kichwa kuwa rahis na vijiwe vya bangii, sorry, nimesema bangili wapi na wapi? Hamkumuona arap Rooter wa kwa njirani akijinoma na mchekeshaji kwa Joji Kichaka akiwatosa wake. Ama kweli…