
Rais Samia: Masanduku yatakavyosema ndivyo matokeo yatakavyokuwa
Dodoma. Rais Samia Suluhu Hassan amepiga kura kuwachagua viongozi wa serikali ya Kijiji cha Chamwino kilichopo Wilaya ya Chamwino jijini hapa, huku akisisitiza wananchi kupiga kura kwa maelewano na kuwa masanduku yatakavyosema ndiyo matokeo yatakavyokuwa. Rais Samia amebainisha hayo wakati akipiga kura leo Jumatano Novemba 27, 2024 katika kituo cha Sokoine kilichopo katika kijiji hicho….