Washtakiwa waomba kubadilishiwa shtaka la mauaji

Dar es Salaam. Mshtakiwa Fadhil Athuman na wenzake wawili, wameiomba Serikali iangalie uwezekano wa kuwabadilishia shtaka la mauaji linalowakabili liwe shtaka la mauaji bila kukusudia. Ombi hilo limetolewa leo Jumatatu, Juni 3, 2024 kupitia wakili wao, Hassan Kiangio wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili washtakiwa kusomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo yaani ‘Committal Proceedings’. Kiangio…

Read More

Wataalamu elimu kujifunza teknolojia mpya

Dar es Salaam. Katika kuhakikisha mpango wa kuwa na mkondo wa elimu ya amali kwa shule za sekondari na vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi unatekelezeka, Tanzania imeweka mkakati wa kuimarisha uhusiano na mataifa yaliyoendelea kwenye teknolojia. Hatua hiyo itawezesha watalaamu wa ndani kujifunza teknolojia mpya zinazotumika kwenye elimu ya ufundi…

Read More

Hivi ndio vipaumbele Wizara ya Afya Zanzibar

Unguja. Wizara ya Afya imeainisha vipaumbele 10 itakavyotekeleza katika bajeti ya mwaka 2024/25 ikiwamo kupunguza vifo vya mama wajawazito kutoka vifo 145 kwa kila vizazi hai 100,000 kwa mwa 2023/2024 na kufika vifo 123 kwa kila vizazi hai 100,000. Kadhalika, kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka vifo 28 kwa kila vizazi hai 1000 na kufikia vifo 26 kwa kila vizazi hai 1000. Kwa mujibu wa…

Read More

Tanroads yawashusha pumzi wakazi Kimara- Ubungo

Dar es Salaam. Wakala wa Taifa wa Barabara Tanzania (Tanroads) imesema upanuzi unaoendelea wa sehemu ya barabara ya Morogoro kutoka Ubungo hadi Kimara-Mwisho jijini Dar es Salaam hautahusisha ubomoaji wa mali za watu. Ujenzi wa sehemu hiyo ni sehemu ya upanuzi wa barabara yote inayounganisha Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam kwa kuibadilisha kuwa…

Read More