WADAU WA TUMBAKU WASIOSHIRIKI USAJILI WA WAKULIMA KUFUNGIWA KAZI – WAZIRI BASHE
Na.Mwandishi Wetu WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, amesema wadau wote wa zao la tumbaku watakaoshindwa kushiriki katika zoezi la usajili wa wakulima hawataruhusiwa kufanya kazi na wakulima, ikiwemo vyama vya ushirika nchini. Mhe. Bashe ametoa kauli hiyo leo, Oktoba 8, 2025, mjini Tabora, wakati wa kikao kazi kilicholenga kuboresha huduma ya bima ya mazao…