
Huduma ya choo Stendi Kuu Mbeya kicheko, wananchi wapongeza na kushauri jambo
Mbeya. Miezi sita tangu Mwananchi kiripoti uhaba na uchakavu wa vyoo katika Stendi Kuu ya Mbeya, Halmashauri ya Jiji hilo limeboresha miundombinu hiyo huku wananchi wakipongeza hatua ya utekelezaji wa haraka. Julai 24, 2024 Mwananchi lilieleza changamoto wanazopitia wananchi wakiwamo wasafiri, wahudumu na watumiaji kwa ujumla wa stendi hiyo wanavyohangaika kupata huduma ya choo. Hata…