
Jaji Tiganga ataka ushiriki wa sekta binafsi udhibiti taka ngumu
Arusha. Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, Joachimu Tiganga ameitaka Serikali kuishirikisha sekta binafsi na kuweka mazingira wezeshi ya kusaidia katika udhibiti wa taka ngumu zinazozagaa mitaani. Jaji Tiganga amesema kuwa zaidi ya tani milioni saba za taka ngumu zinazozalishwa nchini, ni asilimia 35 pekee ndizo zinazokusanywa na kuteketezwa, huku zingine…