
MTU WA MPIRA: Aziz KI na mtihani mwingine kwa Yanga
STEPHANE Aziz Ki. Fahari ya Yanga kwa sasa. Amekuwa na msimu bora kuliko wakati mwingine wowote kwenye maisha yake ya soka. Amemaliza msimu akiwa kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara. Amefunga mabao 21. Ni miaka minne tangu mchezaji wa mwisho alipofunga mabao zaidi ya 20 kwenye msimu mmoja wa Ligi. Alikuwa Meddie Kagere wa…