
Wadau waitaka Serikali iwajibike kuwalinda wenye ualbino
Dar es Salaam. Zikiwa zimepita siku sita tangu kunyakuliwa kwa mtoto mwenye ualbino, Asimwe Novatus (2) na watu wasiojulikana kijijini kwao Bulamula mkoani Kagera, baadhi ya wadau wameshauri kuwe na mikakati endelevu ya kuwalinda watu wenye ulemavu huo. Asimwe alinyakuliwa kwenye mikono ya mama yake Mei 30, 2024 katika Kijiji cha Bulamula, Kata ya Kamachumu,…