
Mrithi wa Dube apatikana Azam FC
AZAM FC imepania. Siku chache baada ya kumtambulisha kiungo, Ever Meza, klabu hiyo imekamilisha dili jingine la kumsajili mshambuliaji mpya, Jhonier Blanco kutoka klabu ya Aguilas Doradas inayoshiriki Ligi Kuu ya Colombia. Straika huyo (24) amesaini mkataba wa miaka minne kuitumikia klabu hiyo kuanzia msimu 2024 hadi 2028. Huo unakuwa usajili wa nne kwa Azam…