
Wananchi wa Afrika Kusini wapiga kura katika uchaguzi mkuu
Wananchi wa Afrika Kusini leo Jumatano wamepiga kura katika uchaguzi mkuu ambao umetajwa kuwa ni muhimu sana kwa nchi hiyo katika kipindi chote cha miaka 30 iliyopita. Chama cha African National Congress kimekuwa madarakani huko Afrika Kusini kwa miongo mitatu sasa. Chama hicho kilifanikiwa kuuangusha utawala wa kikatili wa wazungu walio wachache mwaka wa 1994….