
Mandonga atamba na ngumi kusanyakusanya Tabora
BONDIA machachari wa ngumi za kulipwa nchini Kareem Mandonga sambamba na wenzao wamepimwa uzito leo kwa ajili ya mapambano yatakayofanyika kesho Jumamosi, huku bondia huyo akitamba na ngumi mpya iitwayo ‘Kusanyakusanya’. Mandonga na wenzao wanatarajia kupigana kesho usiku katika ‘Usiku wa Mabingwa wa Tabora’ ambapo Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Upendo Belti Wella kwa niaba…