
Mradi wa maji Same – Mwanga 90% ya utekelezaji, Aweso awasha pump kusukuma maji kwenda tenki la mwisho.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ametembelea na kukagua mradi wa maji Same Mwanga Korongwe ambao umefikia asilimia 90 ya utekelezaji wake ambapo ameshuhudia mifumo ya kutibu maji imekamilika na kisha akafanya zoezi la kuwasha pump za kusukuma maji kupeleka kwenye Tank kubwa la Maji la Kiverenge. Sambamba na hilo Mhe. Aweso ametembelea pia eneo…