DPP amfutia kesi Dk Slaa, aachiwa huru

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemfutia kesi mwanasiasa Mkongwe nchini, Dk Wilibrod Slaa (76) baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kuieleza Mahakama kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya mshtakiwa huyo. Mshtakiwa huyo alikuwa anakabiliwa na shitaka moja la kusambaza taarifa za uongo katika Mtandao wa X kinyume…

Read More

Chaumma yatoa fomu kwa wagombea ubunge Kilimanjaro

Moshi. Chama cha ukombozi wa umma (Chaumma), Mkoa wa Kilimanjaro kimezindua shughuli ya uchukuaji wa fomu wa nafasi za ubunge na madiwani katika mkoa huo, huku watiania katika majimbo saba kati ya tisa wakichukua fomu hizo za ubunge. Waliochukua fomu za  ubunge ni Gervas Mgonja, Jimbo la Same Magharibi, Grace Kiwelu (Vunjo),  Michael Kilawila (Moshi…

Read More

KenGold yachafua hali ya hewa!

KWA wanachoendelea kufanya KenGold kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo ni kama ‘kuchafua hali ya hewa’. Hiyo inatokana na majembe inayoyashusha baada ya kutembeza fagio la nyota wanane ilioanza nao msimu huu ambao ni wa kwanza kushiriki Ligi Kuu. Hadi sasa timu hiyo imetangaza kuachana na Poul Materraz, Asanga Stalon, James Msuva, Steven Mganga,…

Read More

Mawakili wa TLS kuwapa msaada wafungwa

Kilombero. Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Damas Ndumbaro amewahakikishia wafungwa katika magereza mbalimbali nchini, kuwa jopo la mawakili kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), litawafikia na kushughulikia changamoto zao za kisheria hususan rufaa. Akizungumza na askari pamoja na wafungwa katika Gereza la Kiberege, wilayani Kilombero, Dk Ndumbaro amesema kupitia kampeni ya Mama Samia Legal…

Read More

Bolt Tanzania Yagawa Discount Inayoitwa “BOLTXSIMBU” Kusherehekea Medali ya Kwanza ya Dhahabu ya Tanzania.

Bolt Tanzania kwa fahari inatangaza kuzindua nambari mpya ya punguzo, SIMBU, kwa heshima ya Alphonce Felix Simbu, aliyefanya historia kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika Mashindano ya Dunia ya Riadha. Ushindi wa Simbu umeiweka Tanzania kwenye ramani ya riadha ya kimataifa, sambamba na mataifa yenye nguvu kama Kenya. Huu si ushindi…

Read More

Serikali haijatoa mwongozo posho za watumishi walio pembezoni

Dodoma. Serikali imesema haijatoa mwongozo mahususi wa kulipa posho ya mazingira magumu kwa watumishi wa kada ya walimu na watumishi wengine wanaopangiwa vituo vya kazi katika mikoa ya pembezoni kutokana na changamoto zinazoweza kujitokeza katika utekelezaji wake. Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deo Sangu ameyasema…

Read More