
PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 25,2024
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 25,2024 Featured • Magazeti About the author
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 25,2024 Featured • Magazeti About the author
Iringa. Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai ameshinda nafasi hiyo kwa mara nyingine. Mungai ameshinda nafasi hiyo baada ya kuzoa kura 45 dhidi ya kura 34 ambazo mpinzani wake, Emmanuel Chengule amepata. Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo John Mrema amesema kila mgombea alipata haki ya kujieleza na kuchaguliwa. Katika…
NA filimbi ya mwisho itapigwa na mwamuzi wa pambano la baadaye leo kati ya Manchester United na Manchester City. Mwamuzi atakayepuliza filimbi hiyo ni Andrew Madley. Baada ya filimbi yake ndio tutajua kwamba Erik Ten Hag wa Manchester Utd ataendelea kubaki kibaruani au vinginevyo. Kuna wanaosema kwamba haijalishi ambacho kitatokea leo Wembley, huenda Ten Hag…
Dar es Salaam. Uchaguzi wa kumpata mwenyekiti wa Mkoa wa Njombe, uliowakutanisha Rose Mayemba na Ahadi Tweve umevunjika baada ya kutokea ugomvi baina ya pande mbili zinazowaunga mkono wagombea hao. Uchaguzi huo umevunjika leo Ijumaa Mei 24,2024 baada ya kutokea sintofahamu iliyosababishwa na wanachama waliodai kuwa kuna baadhi ya wajumbe kutoka Wilayani Makete hawakupaswa kushiriki…
Dodoma. Wabunge wamecharuka kuhusu migogoro ya ardhi na ucheleweshaji wa fidia kwa wananchi wanaopisha maeneo kwa ajili ya miradi. Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara ametaja vifo na majeruhi waliotokana na fidia isiyo na masilahi kwa wananchi wanaopisha maeneo ya uchimbaji. Wabunge wameeleza hayo wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba…
Dodoma. Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limewataka wazazi wa vijana wanaoitwa kujiunga na mafunzo kwa mujibu wa sheria mwaka 2024 wasikubali kutapeliwa kwa kutozwa fedha. Vijana waliomaliza kidato cha sita mwaka huu, wametakiwa kuripoti katika kambi za JKT kuanzia Juni Mosi hadi 7, 2024. Akizungumza leo Mei 24, 2024, Mkuu wa Tawi la Utawala wa…
Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amewataka wafanyabiashara mkoani humo, kuachana na migomo kabla ya kufanya mazungumzo na viongozi wa mamlaka. Amesema kufanya hivyo ni kutaka kuichafua Serikali. Kauli hiyo ya Homera inakuja ikiwa ni siku moja tangu wafanyabiashara wa maduka katika soko la Mwanjelwa kugoma kufungua maduka yao, wakidai kunyanyaswa na Mamlaka…
Mwanza. Ili kukabiliana na changamoto ya ajira nchini, Serikali kupitia Wizara ya Uvuvi na Mifugo, imetenga Sh10.5 bilioni kwa ajili ya kuwezesha mitaji na miradi ya vijana. Kauli hiyo imetolewa leo Mei 24, 2024 na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi kwenye hafla ya kufunga mafunzo kwa…
SIMBA wana Ladack Chasambi wamoto na KMC wanatambia Wazir Junior. Shughuli ipo kesho kwenye Uwanjwa Sheikh Amri Abeid. Ni wachezaji wawili wazawa ambao katika wiki za hivikaribuni takwimu zao zinavutia viwanjani na leo wanaingia uwanjani kiloa mmoja akibeba ramani ya timu yake. Hii itakuwa mechi ya 12 kwa Simba kukutana na KMC katika ligi huku…
Dar es Salaam. Wajumbe wa mkutano mkuu wa kanda nne za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wana kibarua kigumu cha kuamua kina nani wawe viongozi wa kanda hizo katika uchaguzi unaoanza leo. Kanda ya Victoria yenye mikoa ya Mwanza, Kagera na Geita inafungua pazia la uchaguzi leo. Kanda zingine ni Serengeti yenye mikoa (Mara,…