Misime: Hakuna kontena la silaha lililoingizwa nchini
Wakati tuhuma za kuingizwa kwa kontena lenye silaha zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, Jeshi la Polisi Tanzania limekanusha taarifa hizo likisema ni madai yasiyo na ukweli. Hayo yameelezwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), David Misime, wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu, Septemba 1, 2025, jijini Dodoma….