
RC BATILDA AWATAKA WAFANYABIASHARA KUTOA USHIRIKIANO KWA TRA WANAPOFANYA ZOEZI LA KUTOA ELIMU YA KODI
Leo tarehe 24.05.2024 Mh. Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Batilda Buriani amewataka wafanyabiashara kutoa ushirikiano wa kutosha kwa timu ya uelimishaji kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo inaendelea kutoa elimu ya kodi mlango kwa mlango kwa wafanyabiashara kwa kuwatembelea katika maeneo yao ya biashara. Amewaomba wafanyabiashara wafunguke kwa TRA ili waweze kusikilizwa na…