
Wanaopisha Uwanja wa Ndege Musoma walalamika kucheleweshewa malipo ya fidia
Musoma. Wamiliki wa nyumba 49 zilizopo jirani na Uwanja wa Ndege katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara, wameiomba Serikali kuharakisha malipo yao ya fidia yanayofikia Sh3.9 bilioni ili waweze kupisha ujenzi na upanuzi wa uwanja huo. Wamiliki hao wamesema tayari nyumba zao zilishafanyiwa tathmini tangu mwaka jana lakini mpaka sasa hawajalipwa na hawajui nini kinaendelea….