
Ndege yapata msukosuko angani, abiria 211 wanusurika kifo
Bangkok. Abiria 211 wamenusurika kifo baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kupata msukosuko angani, ikiwa ni saa 10 tangu iliporuka, huku abiria mmoja akifariki dunia jana Jumanne Mei 21, 2024. Abiria hao waliokuwa wakisafiri na ndege ya Shirika la Singapore Airlines kutoka London, Uingereza kwenda Singapore, walijawa na hofu kwenye tukio hilo ambapo abiria 30 wamejeruhiwa….