
Aliyehukumiwa kifungo miaka 30 jela kwa unyang’anyi aachiwa huru
Arusha. Mahakama ya Rufani Tanzania imemwachia huru, Grace Omary aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka 30 jela alichohukumiwa kwa kosa la kumpora mwanamke mwenzake fedha taslimu Sh300,000 kwa kutumia silaha baada ya kushinda rufaa yake. Grace ambaye alijiwakilisha mwenyewe kortini, alihukumiwa kifungo hicho na Mahakama ya Wilaya ya Tarime, akakata rufaa Mahakama Kuu lakini akakwaa kisiki…